KLABU
ya Manchester United inataka kumsajili beki wa St Etienne, Kurt Zouma
lakini inaaminika kinda huyo wa umri wa miaka 19 anaweza kutua Chelsea.
Chipukizi
huyo alisema mapema mwezi huu kwamba kocha Jose Mourinho alizugumza
naye binafsi kwa simu juu ya kuhamia London na klabu hiyo ya Stamford
Bridge iko tayari kutoa Pauni Milioni 12.
United
wanafikiri Chelsea imesitisha nia ya kumchukua, lakini habari za ndani
zinasema wametoa ofa ya kumsaini kwa mkataba wa miaka mitano Zouma
ambaye ni beki wa kati.
Anatakiwa: Beki wa St Etienne, Kurt Zouma (kushoto) anaweza kutua Chelsea

Mzee wa mipango: Jose Mourinho anataka kusajili kinda mwenye kipaji Chelsea, Zouma.
Zouma,
ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10 kwa kumvunja
mchezaji mwenzake mguu, alitarajiwa kuichezeawa timu yake dhidi ya
Bordeaux jana, lakini hakucheza baada ya kulalamika anaumwa, kiasi cha
kushindwa kufanya mazoezi Alhamisi na ijumaa.

Tishio: Zouma katika mechi dhidi ya Bordeaux, huyu ni mmoja wa mabeki wanaotarajiwa kuwa hodari na kutamba Ulaya
Post a Comment