KIUNGO
wa Manchester City na Ivory Coast, Yaya Toure anaamini haheshimiki kama
mmoja wa wanasoka bora duniani kwa sababu ni Mwafrika.
Toure
amefunga mabao 22 msimu huu, akiisaidia City kushinda Kombe la Ligi na
kuendelea kuwamo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Mchezaji mwenzake wa City, Samir Nasri amesema Toure angefurahia kama mmoja wa viungo bora duniani kama asingekuwa Mwafrika.
Hana furaha: Yaya Toure amesema hachukuliwi kama mmoja wa wachezaji bora duniani kwa sababu ya Uafrika wake
Alipoulizwa
nini anachofikiria, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, Toure
alisema: "Nafikiri kitu alichosema Samir ilikuwa ni ukweli kabisa,".
Katika
mahojiano maalum na Football Focus ya BBC World News, Toure alisema
anafikiri hajapata heshima ya kutosha kulingana na mafanikio yake.
Toure
ametwaa mataji ya Ligi Kuu katika nchi nne alizocheza - Ivory Coast,
Ugiriki, Hispania na England - na alikuwemo kwenye kikosi cha Barcelona
kilichotwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2009.
"Kwa
kweli, heshima haswa inakuja kutoka kwa mashabiki,"alisema Mwanasoka
huyo bora Afrika mara tatu. "Sitaki kuwa mgumu na sitaki kuwa tofauti,
lakini nataka kuwa mkweli,".
Toure anafikiri vyombo vya habari vinapaswa kuwapromoti zaidi wanasoka wa Afrika.
"Ikiwa tunacheza vizuri na hatupati heshima kwenye vyombo vya habari, hatuwezi kufika tunapotaka,"alisema. "Watu wanachukuliwa watu wa Afrika kama wanyama,".

Heshima: Toure alikabidhiwa tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika wa Mwaka mapema mwaka huu nchini Nigeria

Mtu babu kubwa: Kiungo huyo anatarajiwa kuiongoza Ivory Coast katika Fainali za Kombe la Dunia

Maneno mazito: Samir Nasri amesema Toure angechukuliwa kama mmoja wa viungo bora duniani iwapo asingekuwa Mwafrika

Kivuli: Toure hana furaha kama ambayo anayo Lionel Messi anayepewa heshima ya mmoja wa wanasoka bora duniani

Taji lingine: Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa ameshika Copa del Rey, naye ameshinda Ballon d'Or mbili
Toure
pia anafikiria wachezaji wa Afrika wanatakiwa kufanya makubwa zaidi ili
kulinganishwa na viungo wa Barcelona, Andres Iniesta na Xavi, ambao
wote ni wachezaji wenzake wa zamani.
Amesema Iniesta na Xavi wanapewa heshima kubwa viungo mahiri wa ushambuliaji, lakini huwa hawashutumiwi wanapochemsha uwanjani.
Toure
amesema amekuwa akisakamwa na vyombo vya habari anaopofanya makosa
uwanjani. Nyota huyo wa Ivory Coast pia hafurahii kwamba Lionel Messi na
Cristiano Ronaldo wanapewa heshima kubwa kama wanasoka bora duniani
peke yao, wakati wachezaji wengine kama wao hawapewi heshima hiyo.
"Ikiwa
utaenda sehemu yoyote ya Afrika kwa sasa, watu watakuambia "ndiyo,
tunamjua yeye [Messi]", lakini ukija Ulaya na useme 'Yaya Toure' watu
watakuambia 'ni nani huyo?' Baadhi watakuambia wanalijua jina langu,
lakini hawaijui sura yangu. Lakini wataijua sura ya Messi,"alisema.
Toure,
ambaye amecheza Ubelgiji, Urusi, Ugiriki, Ufaransa, Hispania na sasa
England, amesema atastaajabu sana kama hatatajwa Mchezaji Bora wa Mwaka
na Chama cha Wanasoka wa kulipwa (PFA).
Ni kati ya wachezaji sita walioingia kwenye orodha ya mwisho, sambamba na Eden Hazard wa Chelsea, Adam Lallana wa Southampton na wachezaji watatu wa Liverpool, Luis Suarez, Steven Gerrard na Daniel Sturridge.
Ni kati ya wachezaji sita walioingia kwenye orodha ya mwisho, sambamba na Eden Hazard wa Chelsea, Adam Lallana wa Southampton na wachezaji watatu wa Liverpool, Luis Suarez, Steven Gerrard na Daniel Sturridge.
Asked
if he would be unhappy not to win the award, Toure replied:
'Definitely. As a champion, as a winner, I always want to win.'

Mweusi pekee aliyeshinda: Mshambuliaji wa zamani wa AC Milan, George Weah ni Mwafrika pekee aliyeshinda Ballon d'Or

Mmaliziaji hodari: Toure amesema mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o ni zaidi ya gwiji kwa mtazamo wake

Washindi! Manchester City wakiwa na taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England chini ya kocha Roberto Mancini msimu wa 2011/12

Angalia hii! Toure akikagua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kocha Pep Guardiola wakati walipokuwa Barcelona mwaka 2009
Alipoulizwa
juu ya Mwafrika mmoja tu kushinda Ballon d'Or hadi sasa- mshambuliaji
wa zamani wa AC Milan na Liberia, George Weah mwaka 1995 - Toure
alielezea pia mambo makubwa yaliyofanywa na wanasoka wengine wa Afrika,
Samuel Eto'o na Didier Drogba katika ngazi ya klabu.
"Hao wachezaji ni zaidi ya magwiji kwangu na kwa Afrika," alisema.
Alipoulizwa
kwamba wachezaji kama Eto'o na Drogba pia wanahisi hawapewi heshima
wanayostahili, mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alijibu: "Kabisa".
Aliongeza:
"Najivunia kuwa Mwafrika, nataka kuwatetea watu wa Afrika na ninataka
kuionyesha dunia kwamba wachezaji wa Afrika wanaweza kuwa wazuri kama wa
Ulaya na Amerika Kusini,".
Post a Comment