KLABU
ya Newcastle United imekamilisha uhamisho wa mkopo wa Facundo Ferreyra
kutoka Shakhtar huku ikiwa fursa ya kumsajili moja kwa moja kwa dau la
Puni Milioni 6.5.
Mshambuliaji
huyo wa Argentina ataiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya Alan Pardew
Uwanja wa St James Park, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
kukataa kurejea klabu yake halisi.
Ferreyra
alikuwa miongoni mwa wachezaji sita wa Shakhtar pamoja na Wabrazil
Douglas Costa, Fred, Dentinho, Alex Teixiera na Ismaily ambao
walishindwa kuripoti Ukraine kufuatia mchezo wa kirafiki dhidi ya Lyon
nchini Ufaransa Jumamosi kutokana na vurugu za kisiasa Ukraine.
Post a Comment