KIUNGO Juan Mata ametambulishwa Manchester United na kukabidhiwa jezi namba nane (8).
Ilitarajiwa
Mspanyola huyo angepewa jezi maarufu Old Trafford, namba saba (7),
afuate nyayo za Cristiano Ronaldo, David Beckham, George Best na Eric
Cantona.
Lakini
mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 37, kiwango kikubwa zaidi
United kutoa kununua mchezaji kihistoria, amechukua namba nane 8,
ambayo mara ya mwisho alivaa Anderson, aliyehamia Fiorentina kwa mkopo.
Tetesi kwenye Twitter zinasema jezi namba saba (7) amewekewa Cristiano Ronaldo atakaporejea mwishoni mwa msimu.

Kijukuu cha mtume: Mashabiki Untied wanaamini jezi namba saba (7) imewekwa kwa ajili ya Cristiano Ronaldo atakaporejea

Wakali:
Ilifikiriwa Mata angepewa jezi namba saba (7) waliyowahi kuvaa nyota
kama George Best, Eric Cantona, David Beckham na Roanldo
Post a Comment