DAKIKA
sita zilitosha kwa Juan Mata kuwadhihirishia Manchester United
hawakukosea kumsajili, baada ya kutengeneza bao la kwanza la timu hiyo
lililofungwa na Robin van Persie katika ushindi wa 2-0 dhidi ya cardiff
City Uwanja wa Old Trafford usiku huu.
Katika
mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, ilibidi kocha David Moyes asuburi
hadi dakika ya 59 kujihakikishia ushindi kwa bao zuri la shley Young.
Matokeo hayo yanaifanya United itimize pointi 40 baada ya kucheza mechi 23, ikibaki nafasi ya saba.
Furaha imerejea: Robin van Persie akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza akirejea kutoka kwenye majeruhi

Ashley Young akishangilia bao lake la pili
Post a Comment