WACHZAJI
wapya wa Cardiff wameanza vizuri baada ya Wilfried Zaha na Kenwyne
Jones kuiwezesha timu hiyo kushinda mabao 2-1 dhidi ya Norwich.
Robert Snodgrass aliifungia Norwich bao la kuongoza dakika ya tano Uwanja wa Cardiff City, lakini Zaha
aliyetua timu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester United, aliyetokea
benchi alimtengenezea nafasi Craig Bellamy kufunga bao la kusawazisha
kipindi cha pili, na Jones akafunga la ushindi dakika kadhaa baadaye.
Post a Comment