WACHEZAJI
wa Manchester United, Danny Welbeck na Tom Cleverley wamepigwa picha
wakicheza disko mtaani wakiwa na demu baada ya timu yao kutolewa katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich.
Mshambuliaji
wa England, Welbeck, mwenye umri wa miaka 23, na mchezaji mwenzake,
Cleverley, mwenye miaka 24, waliserebuka katikati ya Jiji la Manchester
hadi saa 9 usiku jana baada ya United kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2
usiku wa Jumatani nchini Ujerumani.
BIN
ZUBEIRY inafahamu United ilirejea jana na kukutana na mapumziko ya siku
10 kwa wachezaji wake wakaweke akili sawa kabla ya safari ya Everton
Jumapili ya Aprili 20.
Mtu mzima Dan: Welbeck (katikati) akimtazama demu mtaani


Wazee wa kujirusha: Welbeck akizungumza na demu (kushoto) na Cleverley (kulia) akifanya vitu vyake kitaani







Usiku mwema: Cleverley akimuaga demu. Ashley Young pia alikuwepo, lakini aliondoka mapema kwa teksi

Pati la kitaani: Welbeck (kwa nyuma) na rafiki zake wakipoza machungu baada ya kutolewa Ulaya
Post a Comment