Watauweza
mfupa uliomshinda fisi? Benchi jipya la Ufundi la Manchester United
kutoka kushoto Phil Neville, Nicky Butt, Paul Scholes na bosi wao, Ryan
Giggs katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya
Ligi Kuu ya England dhidi ya Norwich City kesho. Giggs ameteuliwa kuwa
kaimu kocha mkuu wa United, baada ya kutimuliwa kwa David Moyes wiki hii
kufuatia matokeo mabaya. Je, timu hii mpya ya benchi la Ufundi
itarejesha furaha kwa Mashetani Wekundu?
Wasifu wao;
Phil Neville: Alijiunga na Man United mwaka 1992 na hadi anastaafu aliichezea mechi 386, akishinda mataji 10, la Kombe Ligi moja, Ligi Kuu sita na Kombe la FA matatu.
Nicky Butt: Alijiunga na Man United mwaka 1991 na hadi anastaafu aliichezea mechi 387 akishinda mataji 10, Kombe la Ligi moja, Ligi Kuu sita na Kombe la FA matatu.
Paul Scholes: Alijiunga na Man United mwaka 1991 na hadi anastaafu ameichezea mechi 718 akishinda mataji 18, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 11 ya Ligi Kuu, matatu ya FA na mawili ya Kombe la Ligi.
Post a Comment