KOCHA
wa Arsene Wenger amepuuza taarifa za kwamba atamtema Joel Campbell
aondoke Arsenal msimu huu, akisema kwamba mshambuliaji huyo kinda yupo
kwenye mipango yake ya msimu ujao.
Nyota
huyo wa Costa Rica mwenye umri wa miaka 22, aliwapagawisha mashabiki
wakati wa Kombe la Dunia nchini Brazil, lakini akawa anahusishwa na
kutolewa kwa mkopo kuelekea msimu ujao.
Wenger amesema atabaki na atacheza michuano ya Kombe la Emirates inayoanza wiki ijayo.

Yuko vizuri: Wenger akizungumza na Waandishi wa Habari jana kuhusu Kombe la Emirates
"Ndiyo,
yeye (Campbell) ni sehemu ya mipango yangu. Anaweza kucheza leo dhidi
ya Benfica,"Wenger aliwaambia Waandishi wa Habari katika mkutano jana.
Post a Comment