MSHAMBULIAJI Dimitar Berbatov amejiunga na Monaco ya Ufaransa kwa mkopo kutoka Fulham hadi mwishoni mwa msimu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33amechagua kuhamia Ligue 1 badala ya kurejea Tottenham iliyomtaka pia.
Vimwaga
fedha Monaco wamemchukua Berbatov azibe pengo la mshambuliaji wao nyota
Radamel Falcao, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita.
Kocha
Rene Meulensteen alikuwa akikimbizana ile mbaya kupata saini ya
mchezaji huyo katika siku ya leo ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo
Ulaya.
Post a Comment