Unknown Unknown Author
Title: CAF YAUPITISHA AZAM COMPLEX KWA MECHI ZA KLABU AFRIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHIRIKISHO  la Soka Afrika (CAF) leo limeupa kibali cha Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,Dar es Salaam unaomilikiwa na klabu ya Azam...
SHIRIKISHO  la Soka Afrika (CAF) leo limeupa kibali cha Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,Dar es Salaam unaomilikiwa na klabu ya Azam Fc kutumika kwa michuano ya klabu barani Afrika .
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo, Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex umekidhi  vigezo vyote vinavyohitajika na CAF kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa.
Moja ya majukwaa ya Azam Complex
Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguzi wake kutoka Zimbabwe, Wilfried Mukuna kuja kukagua Uwanja huu na akawasilisha ripoti CAF, ambayo imefanya shirikisho hilo litoe kibali hicho.
Uongozi wa Azam FC umemshukuru Mukuna, TFF chini ya Rais wake, Jamal Malinzi na uongozi wa CAF, yenye makao yake makuu Cairo, Misri hasusan Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa uwazi na weledi wa hali ya juu.
Azam FC pia inawataarifu wapenzi wake kwamba kuanzia msimu huu mechi zake za Kombe la Shirikisho zitafanyika Uwanja huo. Azam itaanza na Ferroviarrio ya Msumbiji mwezi ujao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

AMANZI "TELEVISION"

 
Top