MECHI
za kwanza za mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinatarajiwa kupigwa wikiendi hii kwa
timu 16 kushuka viwanjani kuwania nafasi nane za makundi mawili.
Inatarajiwa
kuwa michuano mikali kutokana na timu madhubuti zilizopo kwenye hatua
hiyo, inayojumuisha timu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa
Afrika.
Kaizer
Chief ni miongoni mwa timu hizo pamoja na mabingwa wa sasa wa Ligi ya
Mabingwa, Al-Ahly ya Misri ambao watamenyana na Difaa El-Jadidi ya
Morocco wikiendi hii katika Uwanja wa Jeshi la Anga wa Cairo.
Ahly
ni miongoni mwa timu saba zilizowahi kushinda mataji ya Afrika
zinazowania nafasi hizo nane dhidi ya timu nane zilizofuzu katika
mchakato wa Kombe la Shirikisho.
AC
Leopards ya Kongo na Etoile du Sahel ya Tunisia zimewahi kubeba taji
hilo la Kombe la Shirikisho, michuano ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa
michuano ya Kombe la Washindi na Kombe la CAF iliyojumuishwa miaka 10
iliyopita.
ASEC
Mimosas imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika sawa na Kaizer Chiefs
ya Afrika Kusini, wakati Horoya ya Guinea na CA Bizertin ya Tunisia
zimewahi kubeba Kombe la Washindi.
Ahly
iliyotolewa katika Ligi ya Mabingwa kwa vipigo vya kustaajabisha vya
nyumbani na ugenini kutoka kwa Al-Ahly Benghazi ya Libya, inapewa nafasi
sasa ya kuzinduka katika Kombe la Shirikisho.
Kaizer
Chiefs imelazimishwa kuhamishia mechi yake na ASEC Mimosas kutoka
Uwanja wa Soccer City hadi Uwanja mwingine Soweto, uitwao Dobsonvill.
Wakati
Chiefs ilitolewa na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
katika Ligi ya Mabingwa, ASEC iliitoa CS Constantine ya Algeria katika
Kombe la Shirikisho.
Klabu
za Tunisia zimetawala miaka 10 ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa
katika mashindano ya klabu barani, ikitoa mabingwa wanne na washindi wa
pili watatu, na Etoile Sahel na Bizertin zinaanzia ugenini wikiendi hii.
Etoile
itaifuata Horoya, ambao ndoto zao za Ligi ya Mabingwa zilizimwa na
klabu nyingine ya Tunisia, CS Sfaxien, na Bizertin itaivaa Nkana mjini
Kitwe, Zambia.
Bayelsa
United, timu ya mwisho ya Nigeria katika mbio za ubingwa wa mataji ya
CAF mwaka huu, itakuwa mgeni wa Sewe San Pedro ya Ivory Coast na
Leopards itakuwa mwenyeji wa Medeama ya Ghana.
Mechi
baina ya timu za Mali tupu, Real Bamako na Djoliba itafanyika Bamako,
wakati Coton Sport ya Cameroon itamenyana na Petro Atletico ya Angola
mjini Garoua kukamilisha mechi nane za kwanza. Mechi za marudiano
zitachezwa wikiendi ya kati ya Aprili 25 na 27 na droo ya makundi ya
Kombe la Shirikisho itapangwa mjini Cairo Aprili 29.
Home
»
»Unlabelled
» KINYANG’ANYIRO CHA KUCHEZA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA CHAANZA WIKIENDI HII
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment