KOCHA
Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji
16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars kwenye
hoteli ya Hill View jijini Mbeya.
Wachezaji
hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma
Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa
pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini
Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo
ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi),
Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona
(Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito
(Manyara).
Washambuliaji
ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala),
Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala).
Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Atanas Fabian
(Mbeya).
Alisema
mpango huu wa kuboresha timu ya Taifa ambayo inadhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ni endelevu na kusisitiza kuwa hata wale 18
walioachwa watafuatiliwa na TFF na kuitwa panapokuwa na mahitaji.
“Hawa wote wapo kwenye database ya TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema kocha Mayanga.
Wachezaji
ha0 waliingia kambini mjini Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya
mazoezi kwa pamoja kwa karibu wiki nne sasa kabla ya kuchujwa.
Wachezaji
16 waliochaguliwa wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka
huu) na kwenda kwenye kambi ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi
ambapo wataungana na wachezaji wa Taifa Stars wa siku zote.
Baadaye watachujwa tena ili ipatikane timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga
mkono utaratibu huu wa maboresho ya Taifa na imewekeza zaidi ya dola
milioni 2 kwa mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu ndio udhamini mkubwa
zaidi ambao Stars imewahi kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.
16 WAPANDISHWA STARS KUTOKA KIKOSI CHA MABORESHO
Title: 16 WAPANDISHWA STARS KUTOKA KIKOSI CHA MABORESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Star...
Post a Comment