Unknown Unknown Author
Title: NI CHELSEA NA ATLETICO MADRID, REAL MADRID NA BAYERN MUNICH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KLABU ya Chelsea itamenyana na Atletico Madrid katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Droo ya Nusu Fainali iliyofanyika leo im...
KLABU ya Chelsea itamenyana na Atletico Madrid katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Droo ya Nusu Fainali iliyofanyika leo imemtupa kocha Jose Mourinho kwa vinara wa Primera Division leaders, ambao wametoa Barcelona katika Robo Fainali.
Real Madrid itamenyana na mabingwa wateteziu, Bayern Munich katika Nusu Fainali nyingine huku mechi za kwanza zikichezwa Aprili 22 na 23 na marudiano wiki inayofuata.
Ikumbukwe kipa tegemeo wa Atletico Thibaut Courtois mwenye umri wa miaka 21 anachezea timu hiyo kwa mkopo kutoka Chelsea.
Mechi za Ulaya: Chelsea iliitoa Paris Saint-Germain katika Robo Fainali
See you in the semi: Atletico Madrid's Thibaut Courtois can face parent club Chelsea in the semi-final

Tutakutana Nusu Fainali: Kipa tegemeo wa Atletico Madrid, Thibaut Courtois anaweza kukutana na klabu iliyomlea Chelsea katika Nusu Fainali

Kuna taarifa kwamba Chelsea imeiruhusu klabu hiyo ya Hispania kumchezesha kipa huyo Mbelgiji katika mechi zote za Nusu Fainali, kwa kulipa kiasi cha Euro Milioni 3 kwa kila mechi.
Pamoja na hayo, UEFA imepinga hilo ikisema ni kinyume cha sheria na imeweka wazi kwamba inatarajia kipa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji atakuwa huru kucheza mechi zote dhidi ya The Blues bila masharti.
Making the draw: Former Portugal star Luis Figo holds up a draw card with the name of Real Madrid on
Anapanga droo: Nyota wa zamani wa Ureno, Luis Figo akiwa ameshika kadi ya droo yenye jina la Real Madrid 

About Author

Advertisement

Post a Comment

AMANZI "TELEVISION"

 
Top