MAKOCHA
wa timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu
Rugamba), Salum Mayanga na mwenzake Niyungeko Alain Olivier wameahidi
burudani ya nguvu kwenye mechi yao itakayochezwa kesho (Aprili 26 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo ya kirafiki ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar itachezeshwa na refa Anthony Ogwayo kutoka Kenya
na itaanza saa 10 kamili jioni. Ogwayo atasaidiwa na Gilbert Cheruiyot
na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya. Mwamuzi wa mezani atakuwa
Israel Mujuni wa Tanzania wakati Kamishna ni Charles Ndagala.
Mayanga
amesema wanatumia mechi hiyo kama sehemu ya maandalizi ya mechi za
mchujo za Kombe la mataifa ya Afrika, na ameahidi kuchezesha baadhi ya
wachezaji waliopatikana kwenye mpango wa maboresho ya Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Naye
Niyungeko amesema amekuja na kikosi imara ambacho pia kitakuwa na
washambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe na Didier Kavumbagu wa Yanga, lengo
lao ni kuhakikisha wanapata ushindi kwa vile Taifa Stars imekuwa
ikiwasumbua kila wanapokutana nayo.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na
kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh.
10,000.
Wakati
huo huo, Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria
maarufu kama Mart Nooij atatambulishwa kwa waandishi wa habri kesho
Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye ukumbi wa
mikutano wa Uwanja wa Taifa.
TAIFA STARS, BURUNDI ZAAHIDI SOKA MARIDADI
Title: TAIFA STARS, BURUNDI ZAAHIDI SOKA MARIDADI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MAKOCHA wa timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba), Salum Mayanga na mwenzake Niyungeko Alain Olivier wame...
Post a Comment