TIMU
ya vijana ya Kenya inatarajiwa kuwasili nchini leo (Aprili 25 mwaka
huu) saa 1 usiku tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania (Ngorongoro
Heroes).
Mechi
hiyo ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 20 itachezwa Jumapili (Aprili 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 na
sh. 5,000.
Kenya
na Ngorongoro Heroes zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa
Machakos wiki tatu zilizopita. Mshindi baada ya mechi ya marudiano
atacheza na Nigeria katika raundi itakayofuata.
Ngorongoro
Heroes inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo chini ya Kocha John
Simkoko. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa
na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka
Sudan.
KENYA YAWASILI KUIVAA NGORONGORO HEROES
Title: KENYA YAWASILI KUIVAA NGORONGORO HEROES
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya vijana ya Kenya inatarajiwa kuwasili nchini leo (Aprili 25 mwaka huu) saa 1 usiku tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania (Ngo...
Post a Comment