KLABU
ya Racing Santander imefungiwa kucheza michuano ya Kombe la Mfalme
mwakani, baada ya wachezaji wake kugomea mchezo wa marudiano wa Robo
Fainali ya michuano hiyo jana usiku, kwa sababu hawajalipwa mishahara
tangu September.
Walifika
uwanjani na wakashiriki taratibu zote kuelekea kuanza mchezo Uwanja
waCampos de Sport de El Sardinero, lakini wakagoma kucheza dhidi ya
Sociedad.
Refa Gil Manzano aliwauliza wachezaji wa Santander kama watacheza na wakasema hapana, hivyo akamaliza mchezo.
Post a Comment